Pages

September 23, 2015

LOWASSA AWASHUKURU WANANCHI WA MASASI KWA MAPOKEZI MAKUBWA ALIYOYAPATIA

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Boma, Mjini Masasi Mkoani Mtwara, kulikifanyika Mkutano wake wa Kampeni za kuomba ridhaa ya wananchi kugombea nafasi, uliofanyika leo Septemba 22, 2015.


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, waliofikia kusikiliza sera zake katika Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015. Ambapo amewashukuru wananchi wa Mji wa Masasi kwa mapokezi makubwa waliyompatia.
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akizungumza machache na wananchi wa Jimbo la Masasi Mjini, Mkoani Mtwara waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.CHANZO OTHMAN MICHUZI
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara, muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Boma, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni, leo Septemba 22, 2015.
Uwanja wa Boma mjini Masasi, palikuwa hapatishi pale Mgombea Urais alipowasili uwanjani hapo.

Mgombea wa Ubunge anaekubalika na wananchi wa Masasi kupitia Mwamvuli wa Chama cha Wananchi CUF, Ismail Makombe (Maarufu kwa Jina la Kundambada), akizungumza machache na wananchi hao waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa kupitia Chama cha NLD, Dkt. Emmanuel Makaidi akiwa ameambatana na Mkewe, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara leo Septemba 22, 2015.
Chademaaaaaa.........
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea karatasi ya Shairi kutoka kwa Msoma Mashairi, Mohamed Ally (kushoto) mara baada ya kughani Shairi lake.

Magambo yenye jumbe mbali mbali.
Sehemu ya Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Mmoja wa Wazee wa Mji wa Masasi, akiendeleo kuchukua taswira kupitia simu yake, katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.
Umati wa Wananchi wa Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara wakiwa katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Boma, leo Septemba 22, 2015.































No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...